Dalili za mimba changaa . | Dalili za mwanzo za mimba .
Dalili
za mimba changa .
Dalili za mwanzo za mimba au dalili za mimba changa ni
zipi ? Dali za mimba changa hutofautina baina ya mtu mmoja na mwengine kutokana
na kuwa miili huwa ina utofauti mkubwa .
Hizi ndizo dalili za mimba changa au dalili za mwanzo
za mimba .
· Kuujihisi
mgonjwa asubuhi ghafla .
Hii
hutokana na kuongezeka kwa hormoni nyingi za mimba kwenye damu yako kama vile
Oestrogen HCG na kadhalika amabazo hukufanya ujihisi mgonjwa .
· Kuhisi
haja ndogo kila baada ya muda mfupi.
Hii hutokana na hormoni
kama vile progesterone ambazo hufanya misuli kwenye utumbo na kibofu kulegea
.Matokeo yake ni kuwa utajihisi haja ndogo kila baada ya muda mfupi.
· Kukosa
hedhi zako kwa wakati unaostahili.
Hedhi huashiria mwanzo
katika mwezi unaofuata wa mzunguko wako .Kukosa hedhi ni dalili ya mwanzo ya
mimba au dalili ya mimba changaa kutokana na kuwa ukosefu wa hedhi huashiria
kuwa yai lilotengezwa lifanikiwa kukutana na mbegu za kiume na kutengeza
mtoto.Hivyo basi ikiwa umekosa hedhi zako ni vyema ukatafute kipimo cha mimba
ili ukapime .
· Kuhisi
kichefuchefu au kutapika .
Kichefuchefu
au kutapika ni dalili ya mwanzo ya mimba au ni dalili ya mimba changaa kutokana
na kuwa mimba husababisha kuongezeka kwa homoni kwenye damu yako .Homoni hizi huifanya
misuli ya tumbo lako itulie hivo basi kusababisha chakula kisagike kwa pole
pole sana .Matokeo yake ni kuwa utajihisi kichefuchefu kikali haswa asubuhi
unapoamka .
· Kujihisi
kiungulia kikali na kuvimbiwa na tumbo .
Kiungulia kikali na kuvimbiwa na
tumbo hutokana na kuwa mimba husababisha homoni kama vile HCG ziongezeke kwenye
mwili wako .Homoni hizi husababisha chakula tumboni kwako kisagike pole pole
hivo basi kusababisha uhisi kiungulia kikali na kuvimbiwa .
· Kujihisi
kuchoka ghafla.
Kuhisi kuchoka ghafla ni dalili ya
mimba changaa au dalili ya mwanzo ya mimba .Dalili hii hutokana na kwanza kuongezeka
kwa homoni katika mwili wako na pili kutokana na kuwa mwili wako unaanza
kutumia madini na nguvu nyingi kujitayarisha kutengueza mtoto.
· Dalili
nyingine ya mwanzo ya mimba changa ni kuhisi kuvurugikiwa .Hii mara nyingi
husababishwa na homoni iitwayo HCG na oestrogen. Homoni hizi huhusishwa san ana
dalili hii .Mara nyingi utajihisi uko na furaha na baaada ya muda mfupi utakua
wajihisi kulia .
· Kupata
hedhi nyepesi sana zenye matone matone .Mara nyingi dalili hii hutokana kuwa
mimba inaunganika na ukuta wa nyumba yam toto. Dalili hii huonekana katika wiki
moja au mbili baada ya kujamiana .